Joel 3

Mataifa Yahukumiwa


1 a“Katika siku hizo na wakati huo,
nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,

2 bnitayakusanya mataifa yote na kuyaleta
katika Bonde la Yehoshafati
Yehoshafati maana yake Bwana huhukumu.

Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao
kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli,
kwa kuwa waliwatawanya watu wangu
miongoni mwa mataifa
na kuigawa nchi yangu.

3 dWanawapigia kura watu wangu
na kuwauza wavulana ili kupata makahaba;
waliwauza wasichana
ili wapate kunywa mvinyo.

4 e“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda. 5 fKwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu. 6 gMliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.

7 h“Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya. 8 iNitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Bwana amesema.
9 jTangazeni hili miongoni mwa mataifa:
Jiandaeni kwa vita!
Amsha askari!
Wanaume wote wapiganaji
wasogee karibu na kushambulia.

10 kMajembe yenu yafueni yawe panga
na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.
Aliye dhaifu na aseme,
“Mimi nina nguvu!”

11 lNjooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,
kusanyikeni huko.

Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!


12 m“Mataifa na yaamshwe;
na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati,
kwa kuwa nitaketi mahali pale
kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

13 nTia mundu,
kwa kuwa mavuno yamekomaa.
Njooni, mkanyage zabibu,
kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa
na mapipa yanafurika:
kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”


14 oUmati mkubwa, umati mkubwa
katika bonde la uamuzi!
Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu
katika bonde la uamuzi.

15 Jua na mwezi vitatiwa giza,
na nyota hazitatoa mwanga wake tena.

16 p Bwana atanguruma kutoka Sayuni
na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;
dunia na mbingu vitatikisika.
Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake,
ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.

Baraka Kwa Watu Wa Mungu


17 q“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mwenyezi Mungu wenu,
nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
Yerusalemu utakuwa mtakatifu;
kamwe wageni hawatavamia tena.


18 r“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,
na vilima vitatiririka maziwa;
mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.
Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana
na kunywesha Bonde la Shitimu.
Au: Bonde la Migunga .


19 tLakini Misri itakuwa ukiwa,
Edomu itakuwa jangwa tupu,
kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,
ambao katika nchi yao
walimwaga damu isiyo na hatia.

20 uYuda itakaliwa na watu milele
na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

21 vHatia yao ya damu, ambayo sijasamehe,
nitasamehe.”

Bwana anakaa Sayuni!
Copyright information for SwhKC